Friday, April 11, 2008

Ndani ya kuta nne, hakuna shahidi...


Mapenzi ni sawa na mgonjwa, lazima apewe Dozii ya uhakika...Sasa wewe unasubiri nini? Mpe dozi mwenzako usimchoshe....atakukimbia...shauri yako....

Nimatumaini yangu wapenzi wasomaji ya mahaba ni wazima wa afya na mnaendelea vema na shughuli zenu za kila siku.Mi nimzima na namshukuru Mungu kwa kunijaali afya njema. Leo napenda kugusia umuhimu wa Romance.

Kabla ya yote unaweza kujiuliza nini maana ya Romance, kwa kulitamka neno Romance nirahisi sana lakini kulijibu ni vigumu, jaribu utaona kama unaweza kusema nini maana ya Romance. Ni kitu ambacho unaweza kufanya na mpenzi wako, wakati mkiwa faragha, unaweza kutumia muda mwingi mkitomasana ama kupeana vitu ambavyo vitawafanya kuwa karibu zaidi. Romance ni muhumu sana katika maisha ya mapenzi, bila romance maisha yako ya mapenzi hayataweza kudumu. Pia romance ni uthibitisho wa kweli katika mapenzi yenu. Inaonyesha mapenzi yako ya kweli na inakusaidia kuwa mpenzi mzuri kwa mwandani wako.

Mara nyingi siku zinavyokwenda watu wengi husahau kuwapa wapenzi wao Romance nzuri ambayo itawavuta karibu na kuwafanya wajisikie furaha kila wanapokuwa mbali na wapenzi wao, hivyo Romance wakati mwingine huvuta hisia za mapenzi hata kama mpo mbali kimwili lakini kifikikra na hisia zinaweza kuwavuta karibu mkakumbukana kwa yale mliyokutendeana siku moja mlipokuwa faragha.

Kuna njia ambazo unaweza kuzifanya kuweka mshumaa wa romance ambao utakuwa ukiwaka moyoni mwako maishani. Ukakufanya usijute kuwa na mwandani wako, utajiona chaguo lako lilikuwa bora zaidi.

Nini cha kufanya kwa mpenzi wako Kila siku?

1. Mwambie mpenzi wako kiasi gani unavyompenda, sio kukaa kimya, atajuaje kwamba unampenda.

2. Mwambie 'Nakupenda sana' hata mara saba kwa siku, atajisikia furaha moyoni na hata kama alikuwa na wasiwasi na wewe sasa utakuwa wakati wakuamini kiasi gani unavyompenda.

3. Tumia angalau muda mchache wa kuwa nae sehemu tulivu mkipota vinywaji baridi na chakula, pia mtalazimika katika sehemu hiyo tulivu mjadili mipango yenu ya maisha, unaweza kutumia hata saa moja kwa mazungumzo au hata zaidi ya saa moja, sio unaenda dakika mbili unaondoka. Atakuona unakuja kumsanifu au unamuwahi mwingine, kama una kazi ya muhimu mweleze taratibu kwamba una kazi, hatabisha kama ni muungwana. Atakusikiliza na mtapanga labda kukutana kesho utakapokuwa na nafasi, tena hakikisha unatafuta muda wa kuwa na mpenzio.

4. Mfanyie Surprise au kitu ambacho hakikutarajia akilini mwake. Unaweza kumletea zawadi nzuri sana, labda simu ya mkononi, nguo ya ndani, au kitu chochote ambacho unajua hakikuwa akilini mwake.

5. Kama mnaishi pamoja, mnapoamka asubuhi unatakiwa umkumbatie mpenzio, mkeo au mumeo. Unaweza kumsifu kwa kazi ya jana ambayo kwa kiasi kikubwa uliifurahia, usimbanie kuhusu suala la kumsifia. Mpe moyo kwamba anayaweza mashamsham ya gadoro, au vipi? mpenzi msomaji.

Nini cha kumfanyia mpenzio kila wiki?

1.Umanatakiwa kupeana miadi ya kwenda mahala tulivu kabisa, mkibadilisha na mawazo. Sio kila siku kuwa chumbani, unachotakiwa ni kubadilisha mazingira. Wakati unapokuwa mnaelekea labda sehemu ya kubadilishana mawazo, usipende kutembea eti, mume nyuma mke mbele, kwani unamwogopa nani? Waonyeshe wale wanaojua kuchukua vya watu kwamba mmejenga ukuta imara wa penzi lenu. Watashindwa kutupa ndoana za kukuteka wewe ama mpenzio, Shikaneni mikono tena mkionyeshana kiasi gani mnapendana.

2. Mfanyia kitu ambacho wote mnaweza kukifurahia kwa kikifanya kwa pamoja.

3 Kama ni mwanamke unaweza kumpikia chakula kizuri ambacho anapendelae kukila, hakikisha chakula hicho kuanzia mapishi hadi kukiandaa mezani ni kazi yako. Sio Umpikie halafu umwambie 'hausigeli' akamwandalie, haipendezi kabisa na hata jisikia kula chakula chako. Siajabu hata siku hiyo ya wikiendi unaweza kumlisha chakula hadi akashiba, sio kazi kumlisha mpenzio, unajua mwanaume ukimnyenyekea hukisikia ni bora na huongeza mapenzi zaidi.Atakudhamini kuliko chochote, atapenda kukuona mara kwa mara.

Mimi binafsi na mlisha mepnzi wangu, kwani nampenda sana. Ninapomlisha chakula akishiba nae hunilisha kwa furaha. Ninapomtamkia nimeshiba basi hunitolea tabasamu nono lililoshiba midomoni mwake.

4. Mpe mpenzio zawadi ya kumshangaza, ambayo unahisi ataipenda na kuifurahia.

5.Fikiria kitu ambacho utamfanyia wiki nyingine, hasa mapenzi. Usifanye mapenzi kila siku na pia hakikisha unabuni njia nyingine mpya ambazo atazipenda na kuzifurahia.

Nini cha kufanya kila mwezi?

1.Unaweza kutoka na mpenzio mkaenda kufanya Shopping na ukamnunulia zawadi nzuri, kama nguo, viatu, nk.

2.Mnaweza kutizama mkanda wa mahaba, angalau mara mbili kwa mwezi. Hakikisha wakati wa kuangalia mkanda, unamwonyesha staili nzuri uzipendazo. Usione aibu kumwambia unaipenda staili moja kati ya mbili, tatu ulizochagua.

3. Unashauriwa kwenda na mpenzio kucheki afya zenu kila baada ya miezi miwili, hii itasaidia kama kuna magonjwa basi yapatiwe tiba, sio unasema unampenda mwenzio lakini mumshauri kupima afya zenu.

4. Muulize kitu ngani labda ambacho umemfanyia bila kujua kama umemuudhi, kwani wakati mwingin e unaweza kumuudhi mwenzio bila kujua na kukaa kimya kwako kutamfanya aendelee kuumia.

Hebu ukiwa na mpenzi wako jaribu kubadilika bwana, sio kukaa kama gogo au ukimaliza mtanange unakimbilia kufuli, la nini, halina kazi tena ukiwa na mwandani wako...hebu mpe faraja nzito.....aliwazike hakuna kubaniana...

2 comments:

Ema said...

Hi nimeipenda bro!
So interesting

Unknown said...

Interesting, shida yaja kwa mwanaume anaedhani anajua kila kitu kitandani na ukijaribu kumwelekeza jinsi ya kukufurahisha ni shida. Halafu mgumu kweli kweli, alivyozoea yeye ndio hivyo hivyo hakuna kubadilika, hadi inakera. wanawake wengine tupo tayari kujaribu new styles ili kufurahiana na wezi wetu ila mwanaume hataki kujaribu style tofauti. Kazi yake ni kukucriticize tu kila wakati. Mwisho wake hapo kitakua nini?